DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO



UTANGULIZI
Wakati wa ujauzito, ni muhimu kutambua dalili za hatari ambazo zinaweza kuwa ishara ya matatizo au shida za kiafya kwa mama mjamzito. Kupata matibabu haraka katika hali hizi ni muhimu kwa afya ya mama na mtoto.

DALILI ZA HATARI WAKATI WA UJAUZITO
KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA UJAUZITO
Kutokwa na damu sehemu za siri Wakati wa ujauzito ni dalili inayoweza kuashiria tatizo kwenye mimba ambalo linapaswa kuchunguzwa na dactari.

MAUMIVU YA MAKALI CHINI YA TUMBO
Maumivu makali au maumivu chini ya kitovu yanaweza kuwa dalili ya tatizo la mimba. Maumivu haya yanaweza kuambatana na kutokwa na damu au bila kutokwa na damu

MAUMIVU MAKALI YA KIFUA
Maumivu makali ya kifua yanapaswa kuchunguzwa kwa umakini,
Kwani yanaweza kuwa ishara ya tatizo la moyo au matatizo mengine ya kiafya yanayohitaji matibabu haraka

MAUMIVU YA MGONGO AU KICHWA
Maumivu ya mgongo au kichwa ya mara kwa mara haswa yakiambatana na kutokwa na damu au shinikizo la juu la damu, yanaweza kuwa ishara ya matatizo ya afya Wakati wa ujauzito

KUPOTEZA FAHAMU AU KUZIRAI
Kupoteza fahamu au kuzirai kunaweza kuashiria matatizo makubwa ya afya Wakati wa mimba

MABADILIKO YA KASI YA MAPIGO YA MOYO
Ikiwa unaona kuwa mapigo yameongezeka sana au kushuka sana, hii inaweza kuwa ishara ya tatizo la moyo au shinikizo la juu la damu damu

HITIMISHO
Ni muhimu kutambua kuwa dalili hizi za hatari zinaweza kuwa ishara ya matatizo yanayohitajika matibabu haraka ili kulinda afya yako na afya ya mtoto wako.
Ikiwa unahofu au wasiwasi wowote kuhusu hali yako Wakati wa mimba, usisite kumwambia dactari wako au kutafuta huduma ya matibabu mara moja. Daktari ataweza kuchunguzwa hali yako na kutoa ushauri na matibabu sahihi.


ASANTENI
